Wednesday, September 5, 2012


KARIBUNI NDUGU WASOMAJI KWENYE BLOG HII  YA MAFUNZO MBALIMBALI KUHUSIANA NA UJASILIAMALI NA MAMBO MENGINE YA KIMAENDELEO.
Je ungependa kuwa mjasiliamali? Kama ndiyo, elimika zaidi.
Kwenye biashara, tusichukulie mambo kirahisi rahisi wengi wameanza vizuri sana biashara, lakini leo hawapo tena.

Wengine wameanza kitambo sana, lakini wako pale pale kila kukicha hawasongi mbele.

Napenda kuwashauri kwamba tusiegemee tu katika mawazo yetu bali tuchanganye na mawazo ya wataalamu ili tufanye biashara kitalaamu na iwe endelevu.

Pia wajasiriamali wenzangu mnapaswa kutafuta na kuchagua watalaamu ili mpate ushauri wa kitalaamu.

Kabla hujaanza kufanya kazi na mtalaamu fanya utafiti mdogo kuhusu uwezo wake, mathalani unaweza kupata majina na anuani za watalaamu kwenye kitabu cha taarifa muhimu za mawasiliano, kitabu cha taifa cha mawasiliano ya kibiashara au hata kwenye google.

Ukiandika mtalaamu wa tasnia ya biashara yako utapata majina mengi tu, inabaki kazi kwako kutafiti na kubaini anayekufaa.

Sasa basi kwa wale wanaotarajia kuongeza biashara nyingine ni dhahiri kwamba awali ulianzisha  kwa bahati tu na pengine hukufuata taratibu za kitalaamu.

Ndugu mjasirimali unapokuwa katika mchakato wa kuanzisha biashara mpya mara hii zingatia yafuatayo na mafanikio yake utayaona.

Kabla hujaanza baada ya kupata wazo la  biashara, jiulize maswali yafuatayo na kuona kama jibu ni NDIYO basi uko vizuri na kama ni HAPANA jitahidi kufanyia kazi kwanza. 


Mjasiriamali
Umewahi kujiuliza kwa mapana kwa nini unaanzisha biashara nyingine?

Je, unataka kumiliki biashara yako kwa shauku kubwa kiasi cha kutumia muda mwingi bila kujua kiasi gani cha faida utapata?
Je, umeainisha aina ya biashara unayotarajia kuianzisha?
Je, umewahi kufanya kazi yoyote ukiwa kama msimamizi au meneja?
Je, umewahi kupata elimu ya ujasiriamali popote pale?

Una akiba yoyote?

Umeweza kuainisha malengo yako kwa miaka mitatu, mitano  mpaka kumi?

Umewahi kulinganisha kipato unachoweza endapo utakuwa umeamua kuanzisha biashara au kuajiriwa?
Je, familia inaunga mkono mipango yako ya biashara?
Je, unajua wapi pa kupata mawazo na bidhaa zaidi?

Je, kuna mpango kazi  wako binafsi na wafanyakazi?

Fedha
Je, umewahi kupambanua vihatarishi (risk) vya biashara unayoanzisha?

Je, unajua ni kiasi gani cha fedha kinahitajika kuanzisha biashara unayotarajia?
Vipi umeainisha kiasi gani cha fedha utawekeza katika biashara hiyo?
Unajua ni karidhi (credit) kiasi gani unaweza kupata kutoka kwa waghavi (suppliers)?
Je, unajua ni wapi utakopa  fedha za kuongeza kwenye mtaji wako ili uweze kuanzisha biashara yako?
Je, umekokotoa unaweza kupata mapato kiasi gani kwa mwaka kutokana na biashara yako?
Je, unaweza kuendelea na kipato kidogo kuliko kawaida ili utumie kiasi kingine kukuza biashara?
Je, umezungumza na benki yako kuhusu mipango ya kuanzisha biashara nyingine?
Kuhusu mbia
Kama unahitaji mbia mwenye fedha, utalaamu au uzoefu kuliko wewe, je, unafahamu namna na wapi pa kumpata ili mfanye biashara pamoja?

Je, unajua faida na hasara za kufanya biashara peke yako, ubia au kampuni?
Wateja na washindani
Je, umeanisha wateja wako wa sasa na wa baadaye?

Je, umeanisha washindani wako?
Umeweza kujiuliza ni kwa nini wateja wanunue bidhaa au huduma yako na siyo kwenda kununua kwa wenzako?
Je, unatambua kwamba biashara nyingi katika eneo lako zinafanya vizuri?
Je, umeweza kutafiti na kujua biashara nyingine kama yako zinafanya vizuri?
Watu wangapi wanaweza kuvutiwa na bidhaa au huduma utakayotoa?
Je, unapenda kuishi karibu na eneo la biashara yako?
Je, una uhakika biashara unayoanzisha inakubalika?

Kama haikubaliki unafikiria kuihamisha au kuanzisha nyingine?


0 coment�rios: